Skip to main content

Posts

TATIZO YA MAJI KISERIAN KUFIKIA KIKOMO

kajiado press

TUSIWASAHAU WATOTO WA MTAANI:MBUNGE MANJE

kajiado press

TUSIWASAHAU WATOTO WA MTAANI:MBUNGE MANJE

kajiado press

MANJE AISHANGAZA DUNIA

kajiado press

Miradi Inahitaji umakinifu ;Mbunge Manje kwa wahandisi

kajiado press

MBUNGE MANJE ASEMA LUGHA KAJIADO KASKAZINI NI MAENDELEO

kajiado press

Mbunge Manje ajitosa ulingoni kuwatumikia wananchi

kajiado press

CHONDE CHONDE WAHALIFU:KAMANDA RASHID ASEMA

Kamanda wa polisi Kajiado Kaskazini Rashid Mohammed ameapa kuimarisha usalama Katika eneo hilo ambalo makundi hasi ya ujambazi yameanza kuchipuka. Akimhakikishia Mbunge wa Kajiado Kaskazini Mheshimiwa Joseph Manje kamanda Mohamed amesema kuwa kupitia maafisa wapya ambao  wanasimamia kituo cha Ongata Rongai na Ngong visa hivyo vitapungua pakubwa. Kwa upande wake mbunge Manje ameirai idara hiyo ya usalama kuwa macho na kuhakikisha raia wako salama na pia mahusiano baina ya idara ya polisi na umma inakuwa sawa iliupashwaji wa taarifa  za kiintelijensia ni wa kuaminika na kwa muda unaofaa.

MANJE ALIPA ADA

Ni afueni kwa wazazi na wanao Kajiado Kaskazini baada ya mbunge Manje kulipa ada kupitia mfuko wa hazina wa CDF maarufu kama basari. Mbunge Manje alizuru baadhi ya mashule ambako wanafunzi tajika waliopitia mchujo katika kamati mbalimbali jimboni wameweza kulipiwa ada.  Aidha huku umma hasa wa Kajiado Kaskazini ukizidi kusubiria tamko kutoka kwa wizara ya elimu kuhusu tarehe rasmi ya kufungua mashule, imemlazimu Mbunge Manje ambaye rekodi yake katika elimu ikizidi kung'aa kujitwika mzigo na kuhakikisha hamna mwanafunzi atakaye salia nyumbani. Ziara hiyo ya kushtukiza imewaacha baadhi ya wazazi wakiwa na furaha hii ni kutokana na utendaji kazi wa mheshimiwa  Manje.  Ali Omar mmoja wa  mzazi katika eneo la Oloolua amepongeza mheshimiwa na kurai kuwa hakuna kiongozi atakaye mbandua Mheshimiwa katika kiti kufuatia maendeleo ambayo yanazidi kupatikana Kajiado Kaskazini kilakuchao. 

KOSA BARAKOA TIWA MBARONI

Naibu Kamishna Kajiado Kaskazini Bwana Tom Anjere atoa agizo la kuwasukuma ndani wadau wanaokaidi masharti ya kujikinga na janga la COVID-19. Taarifa hii ni kufuatia shinikizo kutoka kwa idara za usalama katika serikali kuu zikirai kuwa janga la Korona ingali inaangamiza watu na maambukizi kuzidi kila kuchao.  Aidha Kaunti ya Kajiado ni miongoni mwa kaunti zilizo andikisha idadi chache ila idara husika imebaini kuwa maeneo ya miji katika kaunti hii yameanza mapuuza na kudhania kuwa hali imerejea kawaidi.  Duru zakuaminika zinasema kuwa endapo raia mwema atapatikana hajavalia barakoa atatiwa mbaroni na kushatakiwa kwa kosa la kuwaweka wakenya hatarani na maambukizi ya KOVIDI 19.  Kwa sasa zoezi limeng'oa nanga nawatuhumiwa watafikishwa  Kortini mnamo siku ya jumatatu na Alhamisi mtawalia. 

SENETA MARY:NINA IMANI NA UHURU

Seneta mteule wa kaunti ya Kajiado Mary Seneta ameapa kuwa yeye ni mwaminifu kwa Mwenyekiti wa chama cha Jubilee rais Uhuru Kenyatta huku akiongeza kuwa hakuwa na maana fishe licha siasa zinaendelea katika chama hiyo.  Akizungumza mbele ya jopo la nidhamu katika chama cha Jubilee inayoongozwa na kinara mkuu wa seneti Irungu Kangata, Seneta Mary anasema kuwa kutokana na utendaji kazi wake katika chama cha TNA hadi sasa wa chama tawala Jubilee kuwa hajawai kiuka  ilani ya chama na utendaji kazi wa chama. Aidha Makataa ya siku 14 imetolewa  kwa maseneta hao ambao wamechukuliwa hatua za kinidhamu ya kutohudhuria mkutano wa chama pale ikulu, hatua ambayo itaeleza hatma ya maseneta hao. Naye kwa upande wake katibu katika chama cha Jubilee Raphael Tuju alisema ipo haja ya heshima kudumu katika chama na wakiukaji kuheshimu muhimili wa uongozi wa taifa. 

500 WAFAIDIKA NA CHAKULA CHA MANJE

Kufuatia tamko la rais Uhuru Kenyatta kuwa mipaka ya Kenya na Nchini jirani kufungwa kwa siku 30 zaidi.Wakaazi wa eneo la Gishagi  katika Jimbo la Kajiado Kaskazini wamepata msaada wa chakula kutoka mbunge wao Mh. Joseph Manje kupitia Wakf wa Manje maarufu kama Manje Foundation. Ajuza na vijana 500 wamefaidika na msaada hiyo ambayo  imewafaidi pakubwa tangu kuzuka kwa janga la Korona. Msaada huo ambayo ni kupitia muungano na Saytha Sai  Ikishirikiana na Wakf wa Manje umesema kuwa zoezi hili litakuwa endelevu na jamii maskini zitazidi kufaidika kupitia kwa msaada  mbalimbali ikiwemo, barakoa na viyeyuzi. Akizungumza mmoja wa wakaazi hao alinena kuwa Mheshimiwa Manje amekuwa akiwa kumbuka maajuza hao na kundi la vijana kila mara kando na mlipuko wa Janga la Korona inchini. 

VIJANA KAJIADO KASKAZINI KUPATA AJIRA

MBUNGE MANJE ADHIBITI CORONA

Maeneo 23 madogo katika jimbo la Kajiado Kaskazini yamenufaika na vituo vya kunawa mikono, pamoja na barakoa zaidi ya 5,000 zilizotolewa katika mfuko wa Hazina ya majimbo maarufu kama NGCDF chini ya usimamizi mkuu wa Mbunge wa Kajiado Kaskazini Mheshimiwa Joseph Manje. Hafla hii ilizinduliwa na Mwenyekiti wa hazina hii mapema hapo jana na kuhakisha kuwa zoezi hili linakuwa endelevu kwa umma.  Kando na taasisi mbalimbali kupendekeza kuwa mbunge wa Kajiado Kaskazini ni miongoni mwa mfuno mwema wa kuigwa kutokana na uchapakazi kazi, baadhi ya majimbo nchini wameomba kupitia muhimili wa bunge kuandaa safari maalum ya kuzuru miradi ambayo mbunge Manje ameanzisha hadi kufikia sasa.  Kadhalika Manje anaema ipo haja ya kusimama kidete na kuhakikisha kuwa Kajiado Kaskazini inapambana na janga la Korona,  kwa sasa visa viwili vilivyo ripotiwa kuwa ni Codiv +  vimebainika kuwa siyo hii ni kwa mujibu wa wizara ya afya kupitia kwa mganga mkuu. 

WE THE COSMOPOLITAN SHARE ON THE BBI

kajiado press

BARAKOA KWA WAJASIRIAMALI

Kufuatia ongezeko kwa maambukizi ya visa vya korona nchini mbunge wa Kajiado Kaskazini Mheshimiwa Joseph Manje alihakikisha kuwa jimbo lake linachukua njia mwafaka ya kujikinga na virusi vya Codiv 19 kwa kusambaza barakoa hasa kwa wafanyabiashara eneo ya Rongai na viunga vyake. Mbunge Manje alisema kuwa ipo haja ya raia kuchukua jukumu ya kujilinda kwa kuzingatia maagizo yanayotolewa na wizara ya afya. "Wahudumu wa bodaboda na wale wa uchukuzi ya umma hakikisheni mnajilinda vyema, pamoja na kuwalinda wateja wenu, vaa barakoa, tumia viyeyuzi na kunawa mikono kwa sabuni" Mbunge Manje alisema. Barakoa zaidi ya 3,000 alizotoa mbunge huyo kama msaada zimetengezwa katika kiwanda cha Vicodec  Rongai na kuundwa kisasa, vilevile mtumiaji anauwezo wa kurudia kuvaa pindi anapotumia, hii ni kutokana na uwezo wa barakoa hizo kufuliwa bila ya kupoteza ubora wake. Ni kauli iliyoungwa mkono na mwenyekiti wa bodaboda rongai aliyesema kwamba janga la Korona limeadhiri biashara hiyo pakubwa kut...

CHAKULA CHA KORONA

Mkurugenzi wa Jubilant Oasis Steward of Africa Bw Jared Oundo. Mkurugenzi wa shirika lisilo la serikali Jubilant Oasis Steward of Africa Bw. Jared Oundo anaomba serikali kutoa mkakati utakao tumika katika kusambaza chakula hasa kwa familia ambazo zimekuwa zikitafuta riziki mida ya usiku. "Vipi kuhusu familia zinazoishi katika vitongoji duni, sasa kama idadi itazidi kuongezeka ya maambukizi na tizamia ujio wa kufunga kila kitu na watu wasalie nyumbani" Jared Oundo asema.  Kwa sasa serikali kupitia wizara ya afya imetoa taadhari kwa umma kuwa virusi vya Korona vinazidi kusambaa mno, hali inayopelekea Maeneo yanayopakana na mji mkuu wa Nairobi  kuandikisha idadi kubwa ya watu walioambukizwa gonjwa la Korona. Kaunti ya Kajiado ikitajwa na maeneo sugu ikiwa ni Kitengala, Rongai na Matasia. Ni hali iliyopelekea wadau hasa watoa maoni ya kisiasa kuhoji na kusihi viongozi kutoa  njia mbadala kuhusu mwafaka wa janga la Korona nchini. 

MANJE AZURU VIZUIZI

  Mbunge wa kajiado kaskazini Joseph Manje amezuru   vizuizi vyilivyopo katika barabara ya Kibiko ,Kona Baridi ,na barabara ya Kiserian Isinya ambazo zinapakana  karibu na maeneo miji ya Nairobi  swala ambalo linahakikisha kuwa visa vya Korona vinazuiwa kusambaa . Ni hatua ambayo  wadau wamepongeza hasa wakati huu wa mlipuko wa ugonjwa wa korona maarufu kama Kovidi -19, hali kadhalika kwa maafisa ambao wanasimamia vizuizi  3 katika eneo bunge la Kajiado Kaskazini wametoa mapendekezo  yao kwa  mbunge huyo namna ya kuboresha huduma kwa wakenya. Aidha Mheshimiwa Manje alihakikisha kuwa hakuna ukandamizaji hasa kwa  wakaazi wanaoishi Kajiado kaskazini wanaopambana kutafuta lishe kwa familia zao.Kwa sasa serikali imeweza kuandikisha Ongezeko kwa idadi ya watu walioambukizwa  Kovid 19. Hatahivyo Kwa upande wake waziri wa usalama wa ndani Fred Matiang'i ametoa agizo na tahadhari kuwa muda wowote  watazuru mipaka mbalimbali nch...

UJUMBE WATOLEWA MSIMU WA PASAKA

TAADHARI KWA VIONGOZI

.. Ni maarufuku na hatari kwa viongozi kutumia janga la Corona kama njia ya kujitafutia umaarufu. Ni kauli iliyochapishwa katika Gatezi la taifa maarufu Kenya Gazette. Tamko hili linajiri baada ya viongozi wa kaunti na maeneo mbunge mbalimbali kutoa ahadi kwa umma kuwa chakula cha msaada kitatolewa. Aidha kwa sasa idadi ya maambukizi COVID - 19 inazidi kuwa  kubwa hali inayopelekea Asilimia 68 ya wakenya kupendekeza kufungiwa kabisaa kwa kila mtu.