Waziri Balala akizungumza na wadau katika sekta ya utalii nchini. Kenya imetenga shilingi milioni 500 katika kusaidia kwenye sekta ya utalii hii nikufuatia hofu ya mlipuko wa COVID 19 maarufu kama Virusi vya Corona . Akizungumza na waandishi wa habari waziri wa utalii anasema hela hizo zitatumika kurejesha imani kwa wadau hasa watalii wa kila mara humu nchini. Kadhalika waziri Balala anasema kuwa hela zingine zitatumika katika kupanga mkakati wa kuhakikisha kero ya virusi vya Korona havisambai kote nchini. "Serikali imetenga shilingi milioni 500 kutoka mfuko wa hazina ya kitaifa ilikuhakikisha kuwa janga la ukosefu wa utalii na kusambaa kwa virusi vya Korona vina kabiliwa vilivyo ."asema waziri Balala.
This is an online platform that publishes timely articles, commentary, reports on current events and issues. It blends traditional journalism with a more personal or informal writing style.