![]() |
Mwanajeshi akimkagua kurutu katika zoezi la kusajili makurutu kwenye jeshi la KDF. |
Kijana mmoja apoteza
maisha katika zoezi linaloendelea la kusajili makurutu katika jeshi (KDF) eneo la Malindi
kaunti ya Kilifi.
”Mwendazake
alikumbana na mauti wakati alipokuwa katika zoezi la kukimbia na kushindwa
kukamilisha mbio na kuzirai gafla
,mafisa wa usajili walijitahidi kumhudumia lakini juhudi zao hazikufua dafu na kijana huyo aliaga dunia.”anasema Luteni
Joseph Nzioka.
Haya yanajiri huku
zoezi hili likizidi kuendelea katika maeneo tofauti humu nchini.
Comments