Ni swala ambalo limeungwa mkono na wazazi pamoja na wadau ambao walikuwa wamekata tamaa na swala la ajira kwa vijana wao hasa Kajiado Kaskazini.
Hali hii imejiri baada ya Mbunge wa Kajiado Kaskazini Mheshimiwa Joseph Manje kurai Bunge la Kitaifa kupitia mswaada uliyotolewa kuwa ipo haja ya serikali kubuni ajira mbalimbali hasa kwa rika la vijana ambao wamesoma lakini hawana ajira rasmi na isiyorasmi.
Mbunge wa Kajiado Kaskazini Kaskazini Manje anasema kuwa hakuna kijana katika jimbo lake atawachwa nje pindi nafasi za ajira kwa vijana zinapojitokeza.
Comments