Mkurugenzi wa shirika lisilo la serikali Jubilant Oasis Steward of Africa Bw. Jared Oundo anaomba serikali kutoa mkakati utakao tumika katika kusambaza chakula hasa kwa familia ambazo zimekuwa zikitafuta riziki mida ya usiku.
"Vipi kuhusu familia zinazoishi katika vitongoji duni, sasa kama idadi itazidi kuongezeka ya maambukizi na tizamia ujio wa kufunga kila kitu na watu wasalie nyumbani" Jared Oundo asema.
Kwa sasa serikali kupitia wizara ya afya imetoa taadhari kwa umma kuwa virusi vya Korona vinazidi kusambaa mno, hali inayopelekea Maeneo yanayopakana na mji mkuu wa Nairobi kuandikisha idadi kubwa ya watu walioambukizwa gonjwa la Korona. Kaunti ya Kajiado ikitajwa na maeneo sugu ikiwa ni Kitengala, Rongai na Matasia.
Ni hali iliyopelekea wadau hasa watoa maoni ya kisiasa kuhoji na kusihi viongozi kutoa njia mbadala kuhusu mwafaka wa janga la Korona nchini.
Comments