Naibu Kamishna Kajiado Kaskazini Bwana Tom Anjere atoa agizo la kuwasukuma ndani wadau wanaokaidi masharti ya kujikinga na janga la COVID-19.
Taarifa hii ni kufuatia shinikizo kutoka kwa idara za usalama katika serikali kuu zikirai kuwa janga la Korona ingali inaangamiza watu na maambukizi kuzidi kila kuchao.
Aidha Kaunti ya Kajiado ni miongoni mwa kaunti zilizo andikisha idadi chache ila idara husika imebaini kuwa maeneo ya miji katika kaunti hii yameanza mapuuza na kudhania kuwa hali imerejea kawaidi.
Duru zakuaminika zinasema kuwa endapo raia mwema atapatikana hajavalia barakoa atatiwa mbaroni na kushatakiwa kwa kosa la kuwaweka wakenya hatarani na maambukizi ya KOVIDI 19.
Kwa sasa zoezi limeng'oa nanga nawatuhumiwa watafikishwa Kortini mnamo siku ya jumatatu na Alhamisi mtawalia.
Comments