Skip to main content

Posts

Showing posts with the label MAKALA
Waziri Balala akizungumza na wadau katika sekta ya utalii  nchini. Kenya imetenga shilingi milioni 500 katika kusaidia kwenye sekta ya utalii hii nikufuatia hofu ya mlipuko wa COVID 19 maarufu kama Virusi vya Corona . Akizungumza na waandishi wa habari waziri wa utalii anasema hela hizo zitatumika  kurejesha imani kwa wadau hasa watalii wa kila mara humu nchini. Kadhalika waziri Balala anasema kuwa hela zingine zitatumika katika kupanga mkakati wa kuhakikisha  kero ya virusi vya Korona havisambai kote nchini. "Serikali imetenga shilingi milioni 500 kutoka mfuko wa hazina ya kitaifa  ilikuhakikisha kuwa  janga la ukosefu wa utalii na kusambaa kwa virusi vya Korona vina kabiliwa vilivyo ."asema waziri Balala.