Maeneo 23 madogo katika jimbo la Kajiado Kaskazini yamenufaika na vituo vya kunawa mikono, pamoja na barakoa zaidi ya 5,000 zilizotolewa katika mfuko wa Hazina ya majimbo maarufu kama NGCDF chini ya usimamizi mkuu wa Mbunge wa Kajiado Kaskazini Mheshimiwa Joseph Manje.
Hafla hii ilizinduliwa na Mwenyekiti wa hazina hii mapema hapo jana na kuhakisha kuwa zoezi hili linakuwa endelevu kwa umma.
Kando na taasisi mbalimbali kupendekeza kuwa mbunge wa Kajiado Kaskazini ni miongoni mwa mfuno mwema wa kuigwa kutokana na uchapakazi kazi, baadhi ya majimbo nchini wameomba kupitia muhimili wa bunge kuandaa safari maalum ya kuzuru miradi ambayo mbunge Manje ameanzisha hadi kufikia sasa.
Kadhalika Manje anaema ipo haja ya kusimama kidete na kuhakikisha kuwa Kajiado Kaskazini inapambana na janga la Korona, kwa sasa visa viwili vilivyo ripotiwa kuwa ni Codiv + vimebainika kuwa siyo hii ni kwa mujibu wa wizara ya afya kupitia kwa mganga mkuu.
Comments
Just saying