![]() |
Katikati ni Mheshimiwa JOSEPH MANJE mbunge wa Kajiado Kaskazini akiwa na wafanyakazi wake hafla ya BBI. |
Hatimaye Mbunge wa Kajiado Kaskazini Joseph Manje amewasilisha mapendekezo ya jimbo analosimamia katika jopo kazi ya BBI mapema hapo jana jijini Nairobi.
Mheshimiwa Manje alisema kuwa ipo haja ya jopo hilo kupokea na kuyafanyia kazi mapendekezo hayo kwa mujibu wa hali ilivyo hasa katika jimbo hilo na kaunti kwa ujumla .
"Nivyema itambulike kuwa watu wengi wanaofanya kazi Nairobi huishi na kutafuta makaazi katika jimbo la Kajiado Kaskazini na maeneo ya karibu hali inayopelekea mabadiliko ya kiuchumi,kisiasa na kadhalika ipo haja ya ujumuishwaji uwepo na uzingatiwe.
Aidha ni matamshi ambayo yaliungwa mkono na Kiongozi Johana Ng'eno ambaye alikuwa anawakilisha wakaazi wa Emurua Dikirr.
Comments