Skip to main content

Posts

Showing posts from 2020

MANJE ALIPA ADA

Ni afueni kwa wazazi na wanao Kajiado Kaskazini baada ya mbunge Manje kulipa ada kupitia mfuko wa hazina wa CDF maarufu kama basari. Mbunge Manje alizuru baadhi ya mashule ambako wanafunzi tajika waliopitia mchujo katika kamati mbalimbali jimboni wameweza kulipiwa ada.  Aidha huku umma hasa wa Kajiado Kaskazini ukizidi kusubiria tamko kutoka kwa wizara ya elimu kuhusu tarehe rasmi ya kufungua mashule, imemlazimu Mbunge Manje ambaye rekodi yake katika elimu ikizidi kung'aa kujitwika mzigo na kuhakikisha hamna mwanafunzi atakaye salia nyumbani. Ziara hiyo ya kushtukiza imewaacha baadhi ya wazazi wakiwa na furaha hii ni kutokana na utendaji kazi wa mheshimiwa  Manje.  Ali Omar mmoja wa  mzazi katika eneo la Oloolua amepongeza mheshimiwa na kurai kuwa hakuna kiongozi atakaye mbandua Mheshimiwa katika kiti kufuatia maendeleo ambayo yanazidi kupatikana Kajiado Kaskazini kilakuchao. 

KOSA BARAKOA TIWA MBARONI

Naibu Kamishna Kajiado Kaskazini Bwana Tom Anjere atoa agizo la kuwasukuma ndani wadau wanaokaidi masharti ya kujikinga na janga la COVID-19. Taarifa hii ni kufuatia shinikizo kutoka kwa idara za usalama katika serikali kuu zikirai kuwa janga la Korona ingali inaangamiza watu na maambukizi kuzidi kila kuchao.  Aidha Kaunti ya Kajiado ni miongoni mwa kaunti zilizo andikisha idadi chache ila idara husika imebaini kuwa maeneo ya miji katika kaunti hii yameanza mapuuza na kudhania kuwa hali imerejea kawaidi.  Duru zakuaminika zinasema kuwa endapo raia mwema atapatikana hajavalia barakoa atatiwa mbaroni na kushatakiwa kwa kosa la kuwaweka wakenya hatarani na maambukizi ya KOVIDI 19.  Kwa sasa zoezi limeng'oa nanga nawatuhumiwa watafikishwa  Kortini mnamo siku ya jumatatu na Alhamisi mtawalia. 

SENETA MARY:NINA IMANI NA UHURU

Seneta mteule wa kaunti ya Kajiado Mary Seneta ameapa kuwa yeye ni mwaminifu kwa Mwenyekiti wa chama cha Jubilee rais Uhuru Kenyatta huku akiongeza kuwa hakuwa na maana fishe licha siasa zinaendelea katika chama hiyo.  Akizungumza mbele ya jopo la nidhamu katika chama cha Jubilee inayoongozwa na kinara mkuu wa seneti Irungu Kangata, Seneta Mary anasema kuwa kutokana na utendaji kazi wake katika chama cha TNA hadi sasa wa chama tawala Jubilee kuwa hajawai kiuka  ilani ya chama na utendaji kazi wa chama. Aidha Makataa ya siku 14 imetolewa  kwa maseneta hao ambao wamechukuliwa hatua za kinidhamu ya kutohudhuria mkutano wa chama pale ikulu, hatua ambayo itaeleza hatma ya maseneta hao. Naye kwa upande wake katibu katika chama cha Jubilee Raphael Tuju alisema ipo haja ya heshima kudumu katika chama na wakiukaji kuheshimu muhimili wa uongozi wa taifa. 

VIJANA KAJIADO KASKAZINI KUPATA AJIRA

MBUNGE MANJE ADHIBITI CORONA

Maeneo 23 madogo katika jimbo la Kajiado Kaskazini yamenufaika na vituo vya kunawa mikono, pamoja na barakoa zaidi ya 5,000 zilizotolewa katika mfuko wa Hazina ya majimbo maarufu kama NGCDF chini ya usimamizi mkuu wa Mbunge wa Kajiado Kaskazini Mheshimiwa Joseph Manje. Hafla hii ilizinduliwa na Mwenyekiti wa hazina hii mapema hapo jana na kuhakisha kuwa zoezi hili linakuwa endelevu kwa umma.  Kando na taasisi mbalimbali kupendekeza kuwa mbunge wa Kajiado Kaskazini ni miongoni mwa mfuno mwema wa kuigwa kutokana na uchapakazi kazi, baadhi ya majimbo nchini wameomba kupitia muhimili wa bunge kuandaa safari maalum ya kuzuru miradi ambayo mbunge Manje ameanzisha hadi kufikia sasa.  Kadhalika Manje anaema ipo haja ya kusimama kidete na kuhakikisha kuwa Kajiado Kaskazini inapambana na janga la Korona,  kwa sasa visa viwili vilivyo ripotiwa kuwa ni Codiv +  vimebainika kuwa siyo hii ni kwa mujibu wa wizara ya afya kupitia kwa mganga mkuu. 

WE THE COSMOPOLITAN SHARE ON THE BBI

kajiado press

BARAKOA KWA WAJASIRIAMALI

Kufuatia ongezeko kwa maambukizi ya visa vya korona nchini mbunge wa Kajiado Kaskazini Mheshimiwa Joseph Manje alihakikisha kuwa jimbo lake linachukua njia mwafaka ya kujikinga na virusi vya Codiv 19 kwa kusambaza barakoa hasa kwa wafanyabiashara eneo ya Rongai na viunga vyake. Mbunge Manje alisema kuwa ipo haja ya raia kuchukua jukumu ya kujilinda kwa kuzingatia maagizo yanayotolewa na wizara ya afya. "Wahudumu wa bodaboda na wale wa uchukuzi ya umma hakikisheni mnajilinda vyema, pamoja na kuwalinda wateja wenu, vaa barakoa, tumia viyeyuzi na kunawa mikono kwa sabuni" Mbunge Manje alisema. Barakoa zaidi ya 3,000 alizotoa mbunge huyo kama msaada zimetengezwa katika kiwanda cha Vicodec  Rongai na kuundwa kisasa, vilevile mtumiaji anauwezo wa kurudia kuvaa pindi anapotumia, hii ni kutokana na uwezo wa barakoa hizo kufuliwa bila ya kupoteza ubora wake. Ni kauli iliyoungwa mkono na mwenyekiti wa bodaboda rongai aliyesema kwamba janga la Korona limeadhiri biashara hiyo pakubwa kut...

CHAKULA CHA KORONA

Mkurugenzi wa Jubilant Oasis Steward of Africa Bw Jared Oundo. Mkurugenzi wa shirika lisilo la serikali Jubilant Oasis Steward of Africa Bw. Jared Oundo anaomba serikali kutoa mkakati utakao tumika katika kusambaza chakula hasa kwa familia ambazo zimekuwa zikitafuta riziki mida ya usiku. "Vipi kuhusu familia zinazoishi katika vitongoji duni, sasa kama idadi itazidi kuongezeka ya maambukizi na tizamia ujio wa kufunga kila kitu na watu wasalie nyumbani" Jared Oundo asema.  Kwa sasa serikali kupitia wizara ya afya imetoa taadhari kwa umma kuwa virusi vya Korona vinazidi kusambaa mno, hali inayopelekea Maeneo yanayopakana na mji mkuu wa Nairobi  kuandikisha idadi kubwa ya watu walioambukizwa gonjwa la Korona. Kaunti ya Kajiado ikitajwa na maeneo sugu ikiwa ni Kitengala, Rongai na Matasia. Ni hali iliyopelekea wadau hasa watoa maoni ya kisiasa kuhoji na kusihi viongozi kutoa  njia mbadala kuhusu mwafaka wa janga la Korona nchini. 

UJUMBE WATOLEWA MSIMU WA PASAKA

TAADHARI KWA VIONGOZI

.. Ni maarufuku na hatari kwa viongozi kutumia janga la Corona kama njia ya kujitafutia umaarufu. Ni kauli iliyochapishwa katika Gatezi la taifa maarufu Kenya Gazette. Tamko hili linajiri baada ya viongozi wa kaunti na maeneo mbunge mbalimbali kutoa ahadi kwa umma kuwa chakula cha msaada kitatolewa. Aidha kwa sasa idadi ya maambukizi COVID - 19 inazidi kuwa  kubwa hali inayopelekea Asilimia 68 ya wakenya kupendekeza kufungiwa kabisaa kwa kila mtu.

KORONA NCHINI

Waziri  wa Afya Mutahi Kagwe . Waziri wa afya Mutahi Kagwe asema kuwa janga la ungonjwa wa Korona huenda ikamwabukiza mtu yoyote kando na dhana inayosambaa kuwa ugonjwa huu ni wa kizungu au watu wenye asili ya uzungu  na bara Asia. Akizungumza mapema leo waziri Mutahi alisema kuwa ugonjwa huo umeripotiwa nchini baada ya binti mwenye asili ya kiafrika umri wa miaka 27 na kutoa taadhari kwa  umma kwa jumla. "Hii leo wizara ya afya imedhibitisha kisa cha binti mwafrika ambaye amepatikana kuwa na virusi vya Korona ambayo imegharimu maisha ya watu wengi ulimwenguni." asema Mutahi Kagwe. Aidha kwa mujibu wa ripoti kutoka wizara hiyo kaunti mbalimbali zipo kwenye hatari ya makali ya virusi hivi.
Waziri Balala akizungumza na wadau katika sekta ya utalii  nchini. Kenya imetenga shilingi milioni 500 katika kusaidia kwenye sekta ya utalii hii nikufuatia hofu ya mlipuko wa COVID 19 maarufu kama Virusi vya Corona . Akizungumza na waandishi wa habari waziri wa utalii anasema hela hizo zitatumika  kurejesha imani kwa wadau hasa watalii wa kila mara humu nchini. Kadhalika waziri Balala anasema kuwa hela zingine zitatumika katika kupanga mkakati wa kuhakikisha  kero ya virusi vya Korona havisambai kote nchini. "Serikali imetenga shilingi milioni 500 kutoka mfuko wa hazina ya kitaifa  ilikuhakikisha kuwa  janga la ukosefu wa utalii na kusambaa kwa virusi vya Korona vina kabiliwa vilivyo ."asema waziri Balala.

MBUNGE MANJE ANENA KUHUSU BBI

Katikati ni Mheshimiwa JOSEPH MANJE mbunge wa Kajiado Kaskazini akiwa na wafanyakazi wake hafla ya BBI. Hatimaye Mbunge wa Kajiado Kaskazini Joseph Manje  amewasilisha mapendekezo ya jimbo analosimamia katika jopo kazi ya BBI mapema hapo jana jijini Nairobi. Mheshimiwa Manje alisema kuwa  ipo haja ya jopo hilo kupokea na kuyafanyia kazi  mapendekezo hayo kwa mujibu wa hali ilivyo hasa katika jimbo hilo na kaunti kwa ujumla . "Nivyema itambulike kuwa watu wengi wanaofanya kazi  Nairobi huishi na kutafuta makaazi katika jimbo la Kajiado Kaskazini  na maeneo ya karibu hali inayopelekea  mabadiliko  ya kiuchumi,kisiasa na kadhalika ipo haja ya ujumuishwaji uwepo na uzingatiwe. Aidha ni matamshi ambayo yaliungwa mkono na Kiongozi Johana Ng'eno  ambaye alikuwa anawakilisha  wakaazi wa Emurua Dikirr.