Mbunge wa kajiado kaskazini Joseph Manje amezuru vizuizi vyilivyopo katika barabara ya Kibiko ,Kona Baridi ,na barabara ya Kiserian Isinya ambazo zinapakana karibu na maeneo miji ya Nairobi swala ambalo linahakikisha kuwa visa vya Korona vinazuiwa kusambaa .
Ni hatua ambayo wadau wamepongeza hasa wakati huu wa mlipuko wa ugonjwa wa korona maarufu kama Kovidi -19, hali kadhalika kwa maafisa ambao wanasimamia vizuizi 3 katika eneo bunge la Kajiado Kaskazini wametoa mapendekezo yao kwa mbunge huyo namna ya kuboresha huduma kwa wakenya.
Aidha Mheshimiwa Manje alihakikisha kuwa hakuna ukandamizaji hasa kwa wakaazi wanaoishi Kajiado kaskazini wanaopambana kutafuta lishe kwa familia zao.Kwa sasa serikali imeweza kuandikisha Ongezeko kwa idadi ya watu walioambukizwa Kovid 19.
Hatahivyo Kwa upande wake waziri wa usalama wa ndani Fred Matiang'i ametoa agizo na tahadhari kuwa muda wowote watazuru mipaka mbalimbali nchini ili kuhakikisha wakenya wanasalia salama bila ya madhara ya gonjwa la Korona ambalo limegharimu maisha ya watu wengi duniani.
Kajiado press.

Comments