![]() |
Mbunge wa Kajiado Kaskazini akigawa chakula mapema mwaka uliopita |
Mbunge wa Kajiado Kaskazini Mheshimiwa Joseph Manje anatarajiwa
kutoa chakula cha msaada kwa familia maskini muda wowote.
Kwa mujibu wa taarifa za ndani ni kwamba Mbunge Manje
anatafuta njia mbadala ya kuwafikishia chakula
hicho hata baada ya serikali kupiga marufuku kurundikana kwa umma.
Hatua hii inajiri baada ya wakaazi katika eneo jimbo
analosimamia wakipambana na hali ngumu ya maisha inayoshuhudiwa kila kuchao.
Aidha serikali ingali inasisitiza umbali wa mita moja hali
inayompa wakati mgumu mbunge Manje ni mbinu ipi itakayo fanikisha ugavi wa
vyakula hivyo kwa jamii maskini.
kajiado press
Comments