Kufuatia ongezeko kwa maambukizi ya visa vya korona nchini mbunge wa Kajiado Kaskazini Mheshimiwa Joseph Manje alihakikisha kuwa jimbo lake linachukua njia mwafaka ya kujikinga na virusi vya Codiv 19 kwa kusambaza barakoa hasa kwa wafanyabiashara eneo ya Rongai na viunga vyake.
Mbunge Manje alisema kuwa ipo haja ya raia kuchukua jukumu ya kujilinda kwa kuzingatia maagizo yanayotolewa na wizara ya afya.
"Wahudumu wa bodaboda na wale wa uchukuzi ya umma hakikisheni mnajilinda vyema, pamoja na kuwalinda wateja wenu, vaa barakoa, tumia viyeyuzi na kunawa mikono kwa sabuni" Mbunge Manje alisema.
Barakoa zaidi ya 3,000 alizotoa mbunge huyo kama msaada zimetengezwa katika kiwanda cha Vicodec Rongai na kuundwa kisasa, vilevile mtumiaji anauwezo wa kurudia kuvaa pindi anapotumia, hii ni kutokana na uwezo wa barakoa hizo kufuliwa bila ya kupoteza ubora wake.
Ni kauli iliyoungwa mkono na mwenyekiti wa bodaboda rongai aliyesema kwamba janga la Korona limeadhiri biashara hiyo pakubwa kutokana na baadhi ya wajasiria mali hao kukosa uwezo wa kununua barakoa kila siku.
Kadhalika idara ya usalama nchini limetoa taadhari kwa wananchi kutonunua maski ovyo kwani matapeli wanatumia maski chafu, maski zilizotiwa dawa kuwahadaa raia.
Comments