Skip to main content

Posts

KORONA NCHINI

Waziri  wa Afya Mutahi Kagwe . Waziri wa afya Mutahi Kagwe asema kuwa janga la ungonjwa wa Korona huenda ikamwabukiza mtu yoyote kando na dhana inayosambaa kuwa ugonjwa huu ni wa kizungu au watu wenye asili ya uzungu  na bara Asia. Akizungumza mapema leo waziri Mutahi alisema kuwa ugonjwa huo umeripotiwa nchini baada ya binti mwenye asili ya kiafrika umri wa miaka 27 na kutoa taadhari kwa  umma kwa jumla. "Hii leo wizara ya afya imedhibitisha kisa cha binti mwafrika ambaye amepatikana kuwa na virusi vya Korona ambayo imegharimu maisha ya watu wengi ulimwenguni." asema Mutahi Kagwe. Aidha kwa mujibu wa ripoti kutoka wizara hiyo kaunti mbalimbali zipo kwenye hatari ya makali ya virusi hivi.
Waziri Balala akizungumza na wadau katika sekta ya utalii  nchini. Kenya imetenga shilingi milioni 500 katika kusaidia kwenye sekta ya utalii hii nikufuatia hofu ya mlipuko wa COVID 19 maarufu kama Virusi vya Corona . Akizungumza na waandishi wa habari waziri wa utalii anasema hela hizo zitatumika  kurejesha imani kwa wadau hasa watalii wa kila mara humu nchini. Kadhalika waziri Balala anasema kuwa hela zingine zitatumika katika kupanga mkakati wa kuhakikisha  kero ya virusi vya Korona havisambai kote nchini. "Serikali imetenga shilingi milioni 500 kutoka mfuko wa hazina ya kitaifa  ilikuhakikisha kuwa  janga la ukosefu wa utalii na kusambaa kwa virusi vya Korona vina kabiliwa vilivyo ."asema waziri Balala.

MBUNGE MANJE ANENA KUHUSU BBI

Katikati ni Mheshimiwa JOSEPH MANJE mbunge wa Kajiado Kaskazini akiwa na wafanyakazi wake hafla ya BBI. Hatimaye Mbunge wa Kajiado Kaskazini Joseph Manje  amewasilisha mapendekezo ya jimbo analosimamia katika jopo kazi ya BBI mapema hapo jana jijini Nairobi. Mheshimiwa Manje alisema kuwa  ipo haja ya jopo hilo kupokea na kuyafanyia kazi  mapendekezo hayo kwa mujibu wa hali ilivyo hasa katika jimbo hilo na kaunti kwa ujumla . "Nivyema itambulike kuwa watu wengi wanaofanya kazi  Nairobi huishi na kutafuta makaazi katika jimbo la Kajiado Kaskazini  na maeneo ya karibu hali inayopelekea  mabadiliko  ya kiuchumi,kisiasa na kadhalika ipo haja ya ujumuishwaji uwepo na uzingatiwe. Aidha ni matamshi ambayo yaliungwa mkono na Kiongozi Johana Ng'eno  ambaye alikuwa anawakilisha  wakaazi wa Emurua Dikirr.

KIFO KAMBINI

Mwanajeshi akimkagua kurutu katika zoezi la kusajili makurutu kwenye jeshi la KDF. Kijana mmoja apoteza maisha katika zoezi linaloendelea la kusajili   makurutu katika jeshi (KDF) eneo la Malindi kaunti ya Kilifi. ”Mwendazake alikumbana na mauti wakati alipokuwa katika zoezi la kukimbia na kushindwa kukamilisha mbio   na kuzirai gafla ,mafisa wa usajili walijitahidi kumhudumia lakini juhudi zao hazikufua dafu na   kijana huyo aliaga dunia.”anasema Luteni Joseph Nzioka. Haya yanajiri huku zoezi hili likizidi kuendelea katika maeneo tofauti humu nchini.

KASHFAA YA PESA NHIF

MKURUGENZI WA BIMA YA TAIFA NHIF GEOFREY GITAU Viongozi 14 kutoka bima ya taifa NHIF watafikishwa  mahakamani  mapema jumanne ilik kujua hatma yao kuhusu kesi inayowakabili inayayohusu ubadhilifu wa fedha na kosa la kutoshirikiana na maafisa jasusi  kuhusu matumizi ya fedha hizo za umma  Mkurugenzi wa mashtaka ya umma Nordin Hajji  katika taarifa kwa  vyombo vya habari alisema  wawili hao Geofrey Gitau ambaye ni mkurugenzi wa  bima ya taifa pamoja na mwenzake  anayesimamia maswala ya fedha na uwekezaji  Wilbert Kiplagat  wanakesi ya kujibu hivyo kulazimika kulala rumande kwa siku ya pili mtawalia ‘’Maafisa walikataa kuwasilisha stakabadhi zinazo orodhesha namna walivyo walipa kampuni ya webtribe mamillioni ya hela.’’anasema hajji.