Kamanda wa polisi Kajiado Kaskazini Rashid Mohammed ameapa kuimarisha usalama Katika eneo hilo ambalo makundi hasi ya ujambazi yameanza kuchipuka.
Akimhakikishia Mbunge wa Kajiado Kaskazini Mheshimiwa Joseph Manje kamanda Mohamed amesema kuwa kupitia maafisa wapya ambao wanasimamia kituo cha Ongata Rongai na Ngong visa hivyo vitapungua pakubwa.
Kwa upande wake mbunge Manje ameirai idara hiyo ya usalama kuwa macho na kuhakikisha raia wako salama na pia mahusiano baina ya idara ya polisi na umma inakuwa sawa iliupashwaji wa taarifa za kiintelijensia ni wa kuaminika na kwa muda unaofaa.
Comments