Skip to main content

Posts

Showing posts from April, 2020

BARAKOA KWA WAJASIRIAMALI

Kufuatia ongezeko kwa maambukizi ya visa vya korona nchini mbunge wa Kajiado Kaskazini Mheshimiwa Joseph Manje alihakikisha kuwa jimbo lake linachukua njia mwafaka ya kujikinga na virusi vya Codiv 19 kwa kusambaza barakoa hasa kwa wafanyabiashara eneo ya Rongai na viunga vyake. Mbunge Manje alisema kuwa ipo haja ya raia kuchukua jukumu ya kujilinda kwa kuzingatia maagizo yanayotolewa na wizara ya afya. "Wahudumu wa bodaboda na wale wa uchukuzi ya umma hakikisheni mnajilinda vyema, pamoja na kuwalinda wateja wenu, vaa barakoa, tumia viyeyuzi na kunawa mikono kwa sabuni" Mbunge Manje alisema. Barakoa zaidi ya 3,000 alizotoa mbunge huyo kama msaada zimetengezwa katika kiwanda cha Vicodec  Rongai na kuundwa kisasa, vilevile mtumiaji anauwezo wa kurudia kuvaa pindi anapotumia, hii ni kutokana na uwezo wa barakoa hizo kufuliwa bila ya kupoteza ubora wake. Ni kauli iliyoungwa mkono na mwenyekiti wa bodaboda rongai aliyesema kwamba janga la Korona limeadhiri biashara hiyo pakubwa kut...

CHAKULA CHA KORONA

Mkurugenzi wa Jubilant Oasis Steward of Africa Bw Jared Oundo. Mkurugenzi wa shirika lisilo la serikali Jubilant Oasis Steward of Africa Bw. Jared Oundo anaomba serikali kutoa mkakati utakao tumika katika kusambaza chakula hasa kwa familia ambazo zimekuwa zikitafuta riziki mida ya usiku. "Vipi kuhusu familia zinazoishi katika vitongoji duni, sasa kama idadi itazidi kuongezeka ya maambukizi na tizamia ujio wa kufunga kila kitu na watu wasalie nyumbani" Jared Oundo asema.  Kwa sasa serikali kupitia wizara ya afya imetoa taadhari kwa umma kuwa virusi vya Korona vinazidi kusambaa mno, hali inayopelekea Maeneo yanayopakana na mji mkuu wa Nairobi  kuandikisha idadi kubwa ya watu walioambukizwa gonjwa la Korona. Kaunti ya Kajiado ikitajwa na maeneo sugu ikiwa ni Kitengala, Rongai na Matasia. Ni hali iliyopelekea wadau hasa watoa maoni ya kisiasa kuhoji na kusihi viongozi kutoa  njia mbadala kuhusu mwafaka wa janga la Korona nchini. 

MANJE AZURU VIZUIZI

  Mbunge wa kajiado kaskazini Joseph Manje amezuru   vizuizi vyilivyopo katika barabara ya Kibiko ,Kona Baridi ,na barabara ya Kiserian Isinya ambazo zinapakana  karibu na maeneo miji ya Nairobi  swala ambalo linahakikisha kuwa visa vya Korona vinazuiwa kusambaa . Ni hatua ambayo  wadau wamepongeza hasa wakati huu wa mlipuko wa ugonjwa wa korona maarufu kama Kovidi -19, hali kadhalika kwa maafisa ambao wanasimamia vizuizi  3 katika eneo bunge la Kajiado Kaskazini wametoa mapendekezo  yao kwa  mbunge huyo namna ya kuboresha huduma kwa wakenya. Aidha Mheshimiwa Manje alihakikisha kuwa hakuna ukandamizaji hasa kwa  wakaazi wanaoishi Kajiado kaskazini wanaopambana kutafuta lishe kwa familia zao.Kwa sasa serikali imeweza kuandikisha Ongezeko kwa idadi ya watu walioambukizwa  Kovid 19. Hatahivyo Kwa upande wake waziri wa usalama wa ndani Fred Matiang'i ametoa agizo na tahadhari kuwa muda wowote  watazuru mipaka mbalimbali nch...

UJUMBE WATOLEWA MSIMU WA PASAKA

TAADHARI KWA VIONGOZI

.. Ni maarufuku na hatari kwa viongozi kutumia janga la Corona kama njia ya kujitafutia umaarufu. Ni kauli iliyochapishwa katika Gatezi la taifa maarufu Kenya Gazette. Tamko hili linajiri baada ya viongozi wa kaunti na maeneo mbunge mbalimbali kutoa ahadi kwa umma kuwa chakula cha msaada kitatolewa. Aidha kwa sasa idadi ya maambukizi COVID - 19 inazidi kuwa  kubwa hali inayopelekea Asilimia 68 ya wakenya kupendekeza kufungiwa kabisaa kwa kila mtu.

MBUNGE MANJE ASAIDIA JAMII MASKINI

Mbunge wa Kajiado Kaskazini akigawa chakula mapema mwaka uliopita Mbunge wa Kajiado Kaskazini Mheshimiwa Joseph Manje anatarajiwa kutoa chakula cha msaada kwa familia maskini muda wowote. Kwa mujibu wa taarifa za ndani ni kwamba Mbunge Manje anatafuta njia mbadala ya kuwafikishia chakula  hicho hata baada ya serikali kupiga marufuku kurundikana kwa umma. Hatua hii inajiri baada ya wakaazi katika eneo jimbo analosimamia wakipambana na hali ngumu ya maisha inayoshuhudiwa kila kuchao. Aidha serikali ingali inasisitiza umbali wa mita moja hali inayompa wakati mgumu mbunge Manje ni mbinu ipi itakayo fanikisha ugavi wa vyakula hivyo kwa jamii maskini.  kajiado press