Skip to main content

Posts

KIFO KAMBINI

Mwanajeshi akimkagua kurutu katika zoezi la kusajili makurutu kwenye jeshi la KDF. Kijana mmoja apoteza maisha katika zoezi linaloendelea la kusajili   makurutu katika jeshi (KDF) eneo la Malindi kaunti ya Kilifi. ”Mwendazake alikumbana na mauti wakati alipokuwa katika zoezi la kukimbia na kushindwa kukamilisha mbio   na kuzirai gafla ,mafisa wa usajili walijitahidi kumhudumia lakini juhudi zao hazikufua dafu na   kijana huyo aliaga dunia.”anasema Luteni Joseph Nzioka. Haya yanajiri huku zoezi hili likizidi kuendelea katika maeneo tofauti humu nchini.

KASHFAA YA PESA NHIF

MKURUGENZI WA BIMA YA TAIFA NHIF GEOFREY GITAU Viongozi 14 kutoka bima ya taifa NHIF watafikishwa  mahakamani  mapema jumanne ilik kujua hatma yao kuhusu kesi inayowakabili inayayohusu ubadhilifu wa fedha na kosa la kutoshirikiana na maafisa jasusi  kuhusu matumizi ya fedha hizo za umma  Mkurugenzi wa mashtaka ya umma Nordin Hajji  katika taarifa kwa  vyombo vya habari alisema  wawili hao Geofrey Gitau ambaye ni mkurugenzi wa  bima ya taifa pamoja na mwenzake  anayesimamia maswala ya fedha na uwekezaji  Wilbert Kiplagat  wanakesi ya kujibu hivyo kulazimika kulala rumande kwa siku ya pili mtawalia ‘’Maafisa walikataa kuwasilisha stakabadhi zinazo orodhesha namna walivyo walipa kampuni ya webtribe mamillioni ya hela.’’anasema hajji.