Seneta mteule wa kaunti ya Kajiado Mary Seneta ameapa kuwa yeye ni mwaminifu kwa Mwenyekiti wa chama cha Jubilee rais Uhuru Kenyatta huku akiongeza kuwa hakuwa na maana fishe licha siasa zinaendelea katika chama hiyo. Akizungumza mbele ya jopo la nidhamu katika chama cha Jubilee inayoongozwa na kinara mkuu wa seneti Irungu Kangata, Seneta Mary anasema kuwa kutokana na utendaji kazi wake katika chama cha TNA hadi sasa wa chama tawala Jubilee kuwa hajawai kiuka ilani ya chama na utendaji kazi wa chama. Aidha Makataa ya siku 14 imetolewa kwa maseneta hao ambao wamechukuliwa hatua za kinidhamu ya kutohudhuria mkutano wa chama pale ikulu, hatua ambayo itaeleza hatma ya maseneta hao. Naye kwa upande wake katibu katika chama cha Jubilee Raphael Tuju alisema ipo haja ya heshima kudumu katika chama na wakiukaji kuheshimu muhimili wa uongozi wa taifa.
This is an online platform that publishes timely articles, commentary, reports on current events and issues. It blends traditional journalism with a more personal or informal writing style.