Waziri wa Afya Mutahi Kagwe . Waziri wa afya Mutahi Kagwe asema kuwa janga la ungonjwa wa Korona huenda ikamwabukiza mtu yoyote kando na dhana inayosambaa kuwa ugonjwa huu ni wa kizungu au watu wenye asili ya uzungu na bara Asia. Akizungumza mapema leo waziri Mutahi alisema kuwa ugonjwa huo umeripotiwa nchini baada ya binti mwenye asili ya kiafrika umri wa miaka 27 na kutoa taadhari kwa umma kwa jumla. "Hii leo wizara ya afya imedhibitisha kisa cha binti mwafrika ambaye amepatikana kuwa na virusi vya Korona ambayo imegharimu maisha ya watu wengi ulimwenguni." asema Mutahi Kagwe. Aidha kwa mujibu wa ripoti kutoka wizara hiyo kaunti mbalimbali zipo kwenye hatari ya makali ya virusi hivi.
This is an online platform that publishes timely articles, commentary, reports on current events and issues. It blends traditional journalism with a more personal or informal writing style.