Mwanajeshi akimkagua kurutu katika zoezi la kusajili makurutu kwenye jeshi la KDF. Kijana mmoja apoteza maisha katika zoezi linaloendelea la kusajili makurutu katika jeshi (KDF) eneo la Malindi kaunti ya Kilifi. ”Mwendazake alikumbana na mauti wakati alipokuwa katika zoezi la kukimbia na kushindwa kukamilisha mbio na kuzirai gafla ,mafisa wa usajili walijitahidi kumhudumia lakini juhudi zao hazikufua dafu na kijana huyo aliaga dunia.”anasema Luteni Joseph Nzioka. Haya yanajiri huku zoezi hili likizidi kuendelea katika maeneo tofauti humu nchini.
This is an online platform that publishes timely articles, commentary, reports on current events and issues. It blends traditional journalism with a more personal or informal writing style.