Ni afueni kwa wazazi na wanao Kajiado Kaskazini baada ya mbunge Manje kulipa ada kupitia mfuko wa hazina wa CDF maarufu kama basari. Mbunge Manje alizuru baadhi ya mashule ambako wanafunzi tajika waliopitia mchujo katika kamati mbalimbali jimboni wameweza kulipiwa ada. Aidha huku umma hasa wa Kajiado Kaskazini ukizidi kusubiria tamko kutoka kwa wizara ya elimu kuhusu tarehe rasmi ya kufungua mashule, imemlazimu Mbunge Manje ambaye rekodi yake katika elimu ikizidi kung'aa kujitwika mzigo na kuhakikisha hamna mwanafunzi atakaye salia nyumbani. Ziara hiyo ya kushtukiza imewaacha baadhi ya wazazi wakiwa na furaha hii ni kutokana na utendaji kazi wa mheshimiwa Manje. Ali Omar mmoja wa mzazi katika eneo la Oloolua amepongeza mheshimiwa na kurai kuwa hakuna kiongozi atakaye mbandua Mheshimiwa katika kiti kufuatia maendeleo ambayo yanazidi kupatikana Kajiado Kaskazini kilakuchao.